1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wauwa watu 11 magharibi mwa Kongo

24 Januari 2024

Wanamgambo wenye silaha waliwaua raia 11 siku ya Jumanne katika eneo la magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa uliokumbwa na migogoro ya kijamii.

https://p.dw.com/p/4bcTa
Kongo, Kinshasa | usalama
Maafisa wa usalama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa kazini.Picha: John Wessels/AFP

Mbunge wa eneo la Kwamouth, Guy Musomo, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia Jumatano (Januari 23) katika kijiji cha Fadiaka.

Ameongeza kuwa wanawake watatu ni miongoni mwa watu waliouawa na amewalaumu wapiganaji wa kundi la Mobondo kwa mauaji hayo.

Mizozo ya ardhi mara nyingi hugeuka kuwa ghasia mbaya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mnamo mwaka 2022, kulizuka ghasia kati ya jamii za Teke na Yaka huko magharibi mwa Kongo.

Jamii ya Teke inajichukulia kuwa wamiliki wa vijiji vilivyo kando ya Mto Kongo, huku jamii ya watu wa Yaka, nayo ikidai kuwa ni wamiliki baada ya kuhamia katika eneo hilo.