1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wauwa watu 11 karibu na Maiduguri Nigeria

Oumilkheir Hamidou
28 Agosti 2019

Wanamgambo wanaoshirikiana na kundi la IS wamewaua wafanyakazi 11 wa ujenzi kaskazini mashariki mwa Nigeria kwa kuwapiga risasi.

https://p.dw.com/p/3Oc60
Maafisa wa usalama wakiwa karibu na eneo linaloshukiwa lilifanywa shambulizi Maiduguri. (Picha ya maktaba)
Maafisa wa usalama wakiwa karibu na eneo linaloshukiwa lilifanywa shambulizi Maiduguri. (Picha ya maktaba)Picha: Reuters/A. Kingimi

Waasi wanaoshirikiana na kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislam-IS wamewapiga risasi na kuwauwa wafanyakazi wa ujenzi 11  kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wengine kadhaa wamejeruhiwa. Mkuu wa wanamgambo hao na wakaazi wa eneo hilo wameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Waasi hao ambao ni wafuasi wa kundi la itikadi kali linalojiita "Dola la Kiislam la mkoa wa magharibi mwa Afrika SWAP waliwafyetulia risasi wafaanyakazi hao katika kijiji cha Wajirko, umbali wa kilomita 150 nje ya mji mkuu wa jimbo la Borno-Maiduguri.

Wanamgambo wa SWAP wanasemekana kuwa na ushawishi mkubwa katika katika eneo la Wajiirko na maeneo ya karibu na hapo unakokutikana msitu wa Sambisa unaodhibitiwa na kundi hasaimu la Boko Haram.