1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wanamgambo wa RSF wadaiwa kupora nyumba na maduka

1 Julai 2024

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa RSF nchini Sudan wanadaiwa kupora nyumba na maduka na kuteka hospitali kuu katika mji wa kati na kuwalazimu maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

https://p.dw.com/p/4hhub
Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa RSF
Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa RSFPicha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa RSF nchini Sudan wanadaiwa kupora nyumba na maduka na kuteka hospitali kuu katika mji wa kati na kuwalazimu maelfu ya watu kukimbia makazi yao. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa wakaazi na mashirika ya ndani ya utetezi wa haki za binadamu.Pande hasimu Sudan zatumia njaa kama silaha - Wataalamu UN

Vikosi vya wanamgambo wa RSF vilianzisha mashambulizi yake dhidi ya wanajeshi wa Sudan katika jimbo la Sennar mapema wiki hii, na kushambulia kijiji cha Jebal Moya kabla ya kuhamia mji mkuu wa mkoa wa Singa, ambako mapigano mapya yamezuka.

Kuzuka kwa mapigano hayo mapya kunazidisha wasiwasi katika vita vya miezi 14 ambavyo vimeisukuma nchi hiyo katika ukingo wa baa la njaa. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu alfu 57,000 wamekimbia nyumba zao kutokana na mapigano hayo.