JamiiBurkina Faso
Wanajeshi 50 wa Burkina Faso wauwawa kwenye shambulizi
21 Februari 2023Matangazo
Taarifa iliyotolewa jana na jeshi la Burkina Faso imesema wanajeshi hao walishambuliwa kwenye jimbo la Oudalan ambalo linaitenganisha nchi hiyo na taifa jirani la Mali.
Shambulizi hilo ambalo linatajwa kuwa limesababisha idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi kwa wakati mmoja tangu kuzuka kwa uasi wa makundi ya itikadi kali nchini humo limetokea siku mbili kabla ya Ufaransa kuhitimisha operesheni zake za kijeshi nchini humo.
Katika mkasa mwingine uliotokea kwenye jimbo lingine la kaskazini mwa nchi hiyo, wanamgambo wenye silaha wamewateka nyara wanawake 50 waliokuwa msituni kutafuta chakula. Serikali imesema imeanzisha msako wa kuwatafuta na kuwaokoa.