1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waliouwawa kwa maandamano Bangladesh wafikia 50

4 Agosti 2024

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mapigano ya leo kati ya waandamanaji wa Bangladesh wanaomtaka Waziri Mkuu Sheikh Hasina ajiuzulu na wafuasi wanaoiunga mkono serikali imeongezeka na kufikia 50.

https://p.dw.com/p/4j66n
Bangladesh Dhaka 2024 | Maandamano ya wanafunzi upya na hatua za polisi
Polisi wakitumia gesi ya kutoa machozi na maguruneti kuwatawanya waandamanaji. Dhaka, Agosti 4, 2024.Picha: Sazzad Hossain/DW

Msemaji wa polisi Kamrul Ahsan Ahsan amesema kumeripotiwa vifo katika maeneo karibu yote ya taifa hilo la Asia ya Kusini ambapo pamoja na idadi hiyo ya vifo inajumuisha polisi 14 na watu wengine 300 wamejeruhiwa.

Maandamano ya Bangladesh yalianza mapemaJulai baada ya kurejeshwa kwa kile kilichofahamika kama mpango wa upendeleo wa ajira, ambao unajumuisha zaidi ya nusu ya kazi zote za serikali.