1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Watu 8 wauawa katika maandamano nchini Bangladesh

4 Agosti 2024

Makabiliano kati ya waandamanaji wa Bangladesh wanaomtaka Waziri Mkuu Sheikh Hasina ajiuzulu na wafuasi wanaounga mkono serikali yamewauwa takriban watu wanane.

https://p.dw.com/p/4j5is
Bangladesh Dhaka | maandamano
Wanafunzi wanashiriki maandamano ya kudai haki kwa waathiriwa waliokamatwa huko Dhaka mnamo Agosti 3, 2024. Picha: Munir Uz Zaman/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa polisi na madaktari, vifo vya vurugu za leo vimetokana na majeraha ya visu na risasi. Taarifa yao inasema watu watatu wameuawa katika wilaya ya kaskazini ya Pabna na wawili katika wilaya ya Rangpur.

Aidha wengine wengine wawili wameuwawa kwenye wilaya ya Mungishanj iliyo katika mji mkuu Dhaka, na muandamanaji mwingine mmoja ameuwawa katika wilaya ya Maghura.