1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 28 wafa maji Mto Kongo

16 Oktoba 2023

Miili ya watu 28 imepatikana kutoka Mto Kongo baada ya mashua waliyokuwamo kuzama kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4XZpm
Demokratische Republik Kongo | Boot auf dem Kongo nahe Mbandaka
Picha: Junior Kannah/AFP/Getty Images

Chrispin Mputu, waziri wa mambo ya ndani wa eneo hilo, amethibitisha idadi ya vifo hivyo na kuliambia shirika la habari la AFP kwamba hadi sasa mamia ya watu bado hawajulikani walipo.

Mputu alisema bado juhudi za uokozi zilikuwa zinaendelea na kwamba idadi jumla ya abiria waliokuwamo katika boti hiyo haijabainika wazi.

Soma zaidi: Raia 18 wauawa na wanamgambo magharibi mwa Kongo

Asasi moja ya kiraia imesema idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

Joseph Boyoko Lokondo, kiongozi wa shirika la kiraia la "Generation consiente" amesema wameorodhesha vifo 50.