1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajue wapinzani wa Yoweri Museveni

18 Februari 2016

Nchini Uganda rais mkongwe Yoweri Museveni anatetea kiti chake dhidi ya wagombea wengine Saba katika uchaguzi mkuu, baaada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 30. Lakini je, wagombea hao ni kina nani hasa?

https://p.dw.com/p/1Hwty
Uganda Präsidentschaftswahlen Kandidaten Mbabazi Besigye Museveni
Kushoto ni Amama Mbabazi, katikati ni Dr. Kizza Besigye na kulia ni rais Yoweri MuseveniPicha: DW/Reuters/picture-alliance/dpa

Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 71 amekuwa rais wa Uganda kwa miaka 30 sasa. Endapo atashinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika leo basi ataanza utawala wa mwongo wake wa nne madarakani

Museveni na Mpinzani wake mkuu daktari Kizza Besigye walikuwa wapiganaji wa msituni waliomtimua Milton Obote maadarakani. Wakati huo Besigye na Museveni walikuwa marafiki wakuu huku Besigye akiwa daktari wa kuaminika wa Museveni

Uhasama wa Museveni na Besigye

Baadaye dr. Besigye akamwoa aliyekuwa mpenzi wa Museveni. Museveni na Besigye wakatofautiana kisiasa pale Besigye alipojiondoa kwenye chama cha National Resistance Movement na kuwania urais mwaka 2001

Huu ni uchaguzi wa nne ambao Besigye anawania urais akitumia chama chake cha Forum for Democratic Change kutaka kumwondoa Museveni mamlakani. Katika majaribio yake yote hajawahi kushinda, matokeo mazuri Besigye kuwahi pata ni wa asilimia 37 ya kura zote alizopata katika uchaguzi wa mwaka 2006

Lawama kadha wa kadha dhidi yake yakiwemo ya uhaini na ubakaji, kushikwa mara kwa mara na polisi na kuwekwa kizuizini, yeye pamoja na wafuasi wake kurushiwa mambomu ya kutoa machozi kando na kuadhibiwa hazijamnyamazisha Dr. Besigye

Uganda Kampala Konvoi Anhänger von Oppositionsführer Kizza Besigye
Picha: Getty Images/AFP/W. Boase

Hata hivyo kura za maoni nchini Uganda zinamweka nyuma ya rais Museveni akiwa na asimia 32 pekee ambazo haziwezi kulazimisha awamu ya pili ya upigaji kura ya urais

Amama Mbabazi ni nani?

Amama Mbabazi mwenye umri wa miaka 67 ni mgombea mwengine wa urais nchini Uganda. Sawa na Museveni na Besigye, Mbabazi pia alikuwa mwanachama wa National Resistance Movement. Alijiondoa kwenye chama hicho alichosaidia kukkijenga pale aliponyimwa nafasi ya kuwa mrithi wa Museveni. Mbabazi ambaye alikuwa katibu mkuu wa NRM kando na kuhudumu kama waziri mkuu alikuwa mtiifu wa miaka mingi kwa chama chake. Alisaidia katika mpango wa kubdili vipengee vya katiba kuhusu muda wa kuhudumu kama rais, hali iliyomwezesha rais Museveni kuendelea kutawala.

Mbabazi ndiye mwanachama mtiifu zaidi ambaye amewahi kumpinga Museveni. Alifanya hivyo pale madai makuu ya ufisadi dhidi yake yalipoibuka, madai ambayo alikanusha. Licha ya kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaosifika Uganda, kampeni zake hazijakuwa na hamasa kubwa. Sawa na Museveni na Besigye, Mbabazi pia anatoka kusini magharibi mwa Uganda

Abed Bwanika mwenye umri wa miaka 48, anawania urais kwa tiketi ya chama cha People´s Development Party(PDP). Amewania urais mara mbili bila kushinda. Licha ya kampeni zake zinazotizamwa kuwa za kiushabiki kutaka kuvutia wengi, wadadisi wanamtizama kama mwanasarakasi kisiasa

Venansius Baryamureeba mwenye umri wa miaka 47 ni mgombea urais wa kibinasi asiyewakilisha chama chochote. Yeye ni mtaalamu wa sayansi na kompyuta na pia mwalimu

Benon Biraro mwenye umri wa miaka 57 ni mwanajeshi mstaafu. Anaongoza chama cha Uganda Farmers Party. Ni mgombea wa urais kwa mara ya kwanza

Mgombea pekee wa kike

Maureen Kyaya mwenye umri wa miaka 41, ndiye mgombea pekee wa kike katika kinyanganyiro cha kuwa rais nchini Uganda. Hii ni mara ya kwanza ambapo anawania urais kama mgombea kibinafsi asiyekiwakilisha chama chochote. Awali Maureen ameshiriki siasa za ndani ya Uganda hasa mashariki ya nchi hiyo

Joseph Mabirizi aliye na umri wa miaka 40 ndiye mgombea aliye na umri mdogo miongoni mwa wagombeaji wote. Amekuwa akifanya kampeni zake kbinafsi huku kauli anayotilia mkazo ni kupambana na ufisadi serikalini

Mwandishi: John Juma

Mhariri: Iddi Ssessanga