1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu waanza sikukuu ya Hijja.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdk7

Mecca, Saudi Arabia.

Mamilioni ya Waislamu wameadhimisha kilele cha ibada ya Hija ya kila mwaka jana kwa kufanya ishara ya kuwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kusimama katika mlima Arafat. Ibada ya kusimama katika mlima Arafat ni imani ya juu kabisa ya kiroho kwa mahujaji, wakati Waislamu wanaamini kuwa Mungu hutoa msamaha kwa kila kitu wakati wa maombi hayo.Mahujaji walifanya ibada yao katika mlima Arafat ambako mtume Mohammad anaamika kuwa alipata sehemu ya mwisho ya maelezo ya kitabu kitakatifu cha Koran.

Katika maeneo ya Afrika mashariki na kati leo ni sikukuu nchini Kenya, Uganda, Burundi na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Akizungumzia sikukuu hii kmkuu wa jumuiya ya Waislamu nchini Burundi Sheikh Salim Issa , alielezea sababu ya leo kuwa ni sikukuu.

Radio Deutsche Welle inawatakia Waislamu wote Idd Mubarak.