1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 6 wamekufa Ufaransa wakijaribu kuingia Uingereza

12 Agosti 2023

Watu sita wamekufa hii leo na wengine kadhaa wameokolewa baada ya boti iliyowabeba wahamiaji kuzama kwenye ujia wa maji unaozitenganisha Uingereza na Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4V67e
Schiffsunglück im Ärmelkanal | Gedenken an 27 Migranten
Picha: PASCAL ROSSIGNOL/REUTERS

Idara inayosimamia usalama kwenye eneo hilo imesema watu wasiopungua 50 ndiyo wameokolewa na ripoti za awali zinasema sita kati yao wapo kwenye hali mahututi.

Waziri Mkuu wa Ufaransa  Elisabeth Borne  alithibitisha kutokea mkasa huo kupitia mitandao ya kijamii na kutuma salamu za pole na rambirambi kwa wahanga wa ajali hiyo.

Soma zaidi: Zaidi ya wahamiaji 100,000 wavuka ujia wa maji wa Uingereza

Mkasa huo umetokea katika wakati chama tawala cha kihafidhina nchini Uingereza kinajaribu kuzuia safari za wahamiaji kupitia ujia huo wa maji kwa hatua za kisera ambazo zimekosolewa kwa kushindwa kupunguza wimbi hilo.

Idadi ya watu wanaojaribu kuvuka  kutoka Ufaransa na kuingia Uingereza kwa kutumia boti dhaifu imeongezeka katika siku za karibuni kutokana na hali nzuri ya hewa.