1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Zaidi ya wahamiaji 100,000 wavuka ujia wa maji wa Uingereza

11 Agosti 2023

Zaidi ya wahamiaji 100,000 wamevuka mpaka wa ujia wa bahari unaoitenganisha Uingereza na Ufaransa kwa kutumia boti.

https://p.dw.com/p/4V4v7
Wahamiaji waliowasili ujia wa maji wa Uingereza
Ujia wa Maji unaoitengenisha Uingereza na Ufaransa umegeuka lango la walanguzi wanaowasafirisha wahamiaji wasio na vibali kuingia UingerezaPicha: SAMEER AL-DOUMY/AFP/Getty Images

Hizo ni takwimu rasmi zilizorekodiwa, tangu Uingereza ilipoanza kuhifadhi data za wahamiaji walioingia kusini mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2018.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imesema kuwa takribani wahamiaji 755 waligunduliwa siku ya Alhamisi kwenye boti 14 wakielekea kwenye pwani ya Uingereza.

Boti hizo kwa mwaka huu zimewaingiza takribani wahamiaji 16,000 na kuifanya idadi jumla ya wahamiaji waliovuka ujia huo kufikia 100,715. Kwa mujibu wa wizara hiyo, afya na ustawi wa kila mmoja aliyeko kwenye boti hizo ni kipaumbele chao kikubwa.