1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiMexico

Wahamiaji 18 wafariki katika ajali ya basi Mexico

7 Oktoba 2023

Watu 18 wamekufa na wengine 27 wamejeruhiwa baada ya basi lililokuwa limewapakia wahamiaji kupinduka kusini mwa Mexico jana Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4XETI
Mexiko Migranten in Ciudad Juárez
Picha: David Peinado/AA/picture alliance

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara kuu inayounganisha mji wa Oaxaca na jimbo jirani la Puebla.

Kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka katika jimbo la Oaxaca de Juárez, watu waliofariki ni wahamiaji kutoka Venezuela, Haiti na Peru waliokuwa wakijaribu kuelekea nchini Marekani.    

Maelefu ya wahamiaji wanaojaribu kuwasili katika eneo la mpaka wa Mexico na Marekani hukabiliwa na hatari ya kutekwa nyara na vikundi vya wahalifu, kuombwa rushwa pamoja na ajali.

Soma pia: Mexico imesema tatizo la wakimbizi haliitishi Mexico pekee bali na mataifa mengine na hivyo kunahitajika nguvu ya pamoja

Kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, zaidi ya wahamiaji 8,200 wamekufa au kutoweka katika bara la Amerika tangu mwaka 2014, wengi wao walipokuwa wakijaribu kufika Marekani kupitia Mexico.