1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMexico

Mexico yaomba mkutano wa kukabili tatizo la wahamiaji

28 Septemba 2023

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador jana Jumatano alitoa mwito wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 10 ya Amerika ya Kusini ili kujadiliana suala la uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4Wt8h
Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador katika picha iliyopigwa Septemba 16, 2023. Kiongozi huyu anataka mkutano wa pamoja ya kuangazia namna ya kudhibiti uhamiaji
Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador katika picha iliyopigwa Septemba 16, 2023. Kiongozi huyu anataka mkutano wa pamoja ya kuangazia namna ya kudhibiti uhamiajiPicha: Fernando Llano/AP Photo/picture alliance

Lopez Obrador amesema hilo si suala linaloisumbua Mexico tu bali ni suala la kimfumo linalotakiwa kushughulikiwa kwa jinsi hiyo. Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa anatarajia pengine mkutano huo utafanyika katika kipindi cha siku kumi zijazo.

Amesema kuna haja ya kuwa na mpango wa pamoja, akiangazia ulinzi wa wahamiaji pamoja na udhibti wa vyanzo vinavyowasukuma watu ambao wengi wao wanatokea Venezuela, Cuba na mataifa ya Amerika ya Kati kuondoka makwao.

Idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakivuka na kuingia Marekani wakitokea Mexico katika wiki za karibuni, na kuongeza shinikizo kwa serikali ya rais Joe Biden juu ya kudhibiti hali hiyo.