Wagombea 19 kuchuana urais Gabon
24 Julai 2023Bongo amepewa kibali licha ya madai ya upinzani kuwa hafai kushikilia wadhifa wa urais.
Alipatwa na kiharusi Oktoba 2018 na akasafirishwa hadi Morocco kwa ajili ya matibabu.
Rais wa Tume ya Uchaguzi ya Gabon Michel Stephane Bonda amesema maombi 27 ya wagombea yalipokelewakabla ya tarehe ya mwisho ya kujaza fomu za uteuzi na 19 yakaidhinishwa.
Soma pia:Rais wa Gabon Ali Bongo kugombea tena urais
Bongo aliingia madarakani katika uchaguzi wenye utata mwaka wa 2009 kufuatia kifo cha baba yake Omar Bonfo na akashinda tena mwaka wa 2016. Anagombea kwa muhula wa tatu baada ya kutawala kwa karibu miaka 14.
Gabon haina ukomo wa mihula ya urais katika katiba yake. Waziri wa zamani wa madini Alexandre Barro Chambrier anaonekana kuwa mpinzani mkuu wa Bongo.
Mwanauchumi huyo mzaliwa wa Paris anashiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa rais.