1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Gabon Ali Bongo kugombea tena urais

10 Julai 2023

Rais wa Gabon Ali Bongo ametangaza jana jioni kuwa atawania tena urais kwa muhula wa tatu kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 26 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4TemA
Gabon Ali Bongo
Rais wa Gabon Ali BongoPicha: Julien de Rosa/AFP

Rais wa Gabon Ali Bongo ametangaza jana jioni kuwa atawania tena urais kwa muhula wa tatu kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 26 mwaka huu. Katiba ya Gabon haina ukomo wa mihula.

Bongo mwenye umri wa miaka 64,ameliongoza taifa hilo la Afrika ya Kati na linalozalisha mafuta kwa mihula miwili ya miaka saba tangu alipomrithi baba yake Omar Bongo aliyefariki mwaka 2009 baada ya kuitawala Gabon tangu mwaka 1967.

Upinzani nchini Gabon umekuwa ukipinga ushindi wa Ali Bongo na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2016 yalizusha vurugu hadi kupelekea jengo la Bunge kuteketea kwa moto. Familia ya Bongo wako madarakani nchini Gabon kwa miaka 56.

Azma yake ya kugombea urais ilitiliwa shaka alipopata kiharusi Oktoba mwaka 2018 na kusafirishwa hadi Morocco kwa matibabu. Alikaa huko miezi mitatu lakini akarudi muda mfupi baada ya kuzimwa jaribio la mapinduzi akiwa nje ya nchi.