1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi kote Ugiriki wagoma kufuatia ajali ya treni

8 Machi 2023

Maelfu ya wafanyakazi watashiriki mgomo wa nchi nzima nchini Ugiriki leo wakiandamana dhidi mkasa mbaya zaidi wa treni kuwahi kutokea nchini humo ambapo watu 57 walifariki dunia.

https://p.dw.com/p/4ONj9
Griechenland Athen | Demo anläßlich des Zugunglücks
Picha: Yorgos Karahalis/AP/picture alliance

Maelfu ya wafanyakazi watashiriki mgomo wa nchi nzima nchini Ugiriki leo wakiandamana dhidi mkasa mbaya zaidi wa treni kuwahi kutokea nchini humo ambapo watu 57 walifariki dunia. Kunatarajiwa kuwa na maandamano makubwa pia nje ya bunge huko Athens.

Mgomo huu utakaowajumuisha wafanyakazi mbalimbali kutoka sekta ya umma, unatarajiwa kutatiza usafiri wa mabasi, treni na hata feri ambazo zitakuwa zimetia nanga bandarini kwani mabaharia nao watajiunga na maandamano hayo. Tangu Alhamis iliyopita wafanyakazi wa reli nchini humo wamegoma wakidai kwamba madai yao ya mazingira ya usalama hayajatiliwa maanani kwa miaka sasa.