1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSyria

Wafadhili waahidi dola bilioni 7 kwa Uturuki, Syria

21 Machi 2023

Umoja wa Ulaya na wafadhili wa kimataifa wameahidi dola bilioni 7.5 za Kimarekani kuzisaidia Uturuki na Syria kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi ya mwezi uliopita ambayo yaliwauwa zaidi ya watu 50,000.

https://p.dw.com/p/4OyDm
Türkei Samandag Erdbeben Ruinen
Picha: Emrah Gurel/AP Photo/picture alliance

Umoja wa Ulaya umesema kongamano hilo lilijumuisha washiriki 400 wa kimataifa, zikiwemo serikali na mashirika yasiyo ya kiraia. Maafisa wa Syria na Urusi hawakualikwa.

Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema euro bilioni 3.3 zitatoka kwa Umoja wa Ulaya wenye nchi 27 wanachama. Halmashauri hiyo pekee itatoa euro bilioni 1 kusaidia katika juhudi za kuijenga upya Uturuki. Von der Leyen amesema euro milioni 108 za ziada zitatumika katika msaada wa kiutu na kuiinua Syria.

Soma pia: Mwezi mmoja tangu tetemeko la ardhi kutikisa Uturuki, Syria

Umoja wa UIaya hauna mahusiano ya kidiplomasia na Rais wa Syria Bashar al-Assad na imeiwekea Damascus vikwazo vikali