1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadau: Balozi wa Rwanda DRC afukuzwe

Admin.WagnerD27 Mei 2022

Miito inaongezeka nchini Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo ya kutaka kufukuzwa kwa balozi wa Rwanda mjini Kinshasa na kusitishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4BwQ0
DRK Symbolbild FARDC
Picha: Alain Wandimoyi/AFP

Hayo yanafuatia madai ya serikali ya Congo kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi wa kundi la M23.

Suala hilo linaonekana kuwaunganisha Wakongomani kwa ujumla bila kujali itikadi  yao ya kisiasa, makundi karibu yote yanasema ni lazima kusimama kama taifa moja ili kutetea maslahi ya Congo dhidi ya uvamizi wa kigeni unaoongozwa na Rwanda.

Vigogo wa muungano wa vyama vilivyo madarakani nchini humo, Union sacrée de la nation (USN), alikosoa vikali njama za kujaribu kuigawa nchi  na  wametoa wito kusitishwa  haraka uhusiano na Rwanda na kuujulisha  Umoja wa Mataifa kuhusu kinachoendelea.

Daniel Oma Lusambo, mmoja wa viongozi wa muungano USN alisema hali ya sasa katika eneo la Mashariki mwa Kongo ni uvamizi mtupu ambao unalengo la kuiligawa taifa hilo lililo kusini mwa jangwa la Sahara.

"Tunashauri kufungwa mara moja  mipaka na Rwanda" Alisema.

Jambo hilo limeungwa mkono pia na upinzani unaotaka kuandaliwa maandamano makubwa nchini kote dhidi ya Rwanda. Augustin Bisimwa ni msemaji wa Bloc Patriotique Crédible du Peuple (BPCP).

Soma zaidi:Ripoti mpya yaonesha machafuko yauwa watu elfu 15 DRC

Alisema  DRC ni wakati mzuri wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia ambayo yapo kwa sasa.

"Serikali imfukuze Balozi wa Rwanda nchini Kongo na kumrudisha nyumbani haraka Balozi wa Kongo nchini Rwanda." Alisisitiza na kuongeza kwamba  serikali ya Kongo iweze kuwapatia wanajeshi uwezo ili wamalize huo uvamizi wa Rwanda katika eneo hilo la mzozo.

Mashirika ya kiraia yaingilia kati kutaka vita kumalizwa

Upande mwengine mashirika za kiraia yalisema muda umewadia kwacongo kuandika historia katika kumaliza mapiganohayo ambayo yamekuwa yakizuka mara kwa mara katika eneo hilo dhidi ya jeshi la nchi na vikundi vya wapiganaji.

Demokratische Republik Kongo | Masisi Provinz | Ankunft Milizenführer Mbura
mwanamke kutoka DRC akiwa na mtutu wa BundukiPicha: Mariel Müller/DW

Aidha yametoa rai kwa  Wakongomani kupigana vita hadi nchini Rwanda ambako wanadai vita hivyo vilipangwa,Christopher Ngoy Mutamba ni mratibu wa mashirika ya kiraia hapa nchini DRC.

"Shirika la kiraia la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linalaumu  vikali jeshi la Rwanda kushiriki kikamilifu katika operesheni"

Soma zaidi:Nia ya Uganda kuondoa wanajeshi DRC yazusha maoni mseto

Alitoa wito kwa wakongomani na kuongeza kwamba ni lazima walisaidie jeshi la nchi yao kwa namna mbalimbali katika kushinda mapigano hayoaliyoyataja kuwa yalipangwa.

Rwanda imeendelea kunyooshewakidole kila mara kwa kuunga mkono waasi mbalimbali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. hata hivyo serikali ya  Kigali imekuwa ikikanusha tuhuma hizo.

Mapigano Mashariki mwa DRC yasababisha watu 10,000 kukimbilia Uganda