1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Wabunge watatu wa upinzani wakamatwa Senegal

7 Februari 2024

Wabunge watatu wa upinzani wamekamatwa nchini Senegal, huku kukiwa na mzozo mkali wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4c7Gg
Senegal - Maafisa wa Polisi wakijaribu kuwadhibiti waandamanaji mjini Dakar
Maafisa wa Polisi nchini Senegal wakizuia barabara inayoelekea Bungeni mjini Dakar ili kujaribu kuwadhibiti waandamanaji wanaopinga hatua ya kuahirishwa uchaguzi wa rais: 05.02.2024Picha: JOHN WESSELS/AFP

Mvutano huo ni kufuatia hatua ya Bunge kupiga kura hapo jana na kuahirisha uchaguzi wa urais hadi Disemba 15 mwaka huu, hatua iliyotajwa na upinzani kuwa  "mapinduzi ya kikatiba".

Miongoni mwa waliokamatwa ni mbunge Guy Marius Sagna ambaye alijaribu siku ya Jumatatu kuzuia zoezi la kuupigia kura mswada huo. Msemaji wa chama cha upinzani kilichofungiwa cha Pastef, El Malick Ndiaye amesema ni wazi sasa kwamba Senegal imeingia katika utawala wa kidikteta.

Hatua hiyo ya kuahirisha uchaguzi imesababisha maandamano makubwa katika miji kadhaa nchini Senegal pamoja na kuzua wasiwasi wa kimataifa kuhusu mustakabali wa nchi hiyo ambayo inachukuliwa kama kinara wa demokrasia huko Afrika Magharibi.