1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabadilisha pasipoti wanasubiri muda mrefu Ujerumani

4 Agosti 2024

Kwa mujibu wa mamlaka za miji nchini Ujerumani wageni wanaoomba pasipoti ya Ujerumani wanakabiliwa na tatizo la kusubiri kwa muda mrefu hata baada ya masharti kulegezwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4j63O
Einbürgerungen | Deutsche Staatsbürgerschaft
Picha: Wolfgang M. Weber/IMAGO

Maombi yanaelezwa kuongezeka baada ya mabadiliko ya taratibu za utoaji wa pasipoti hizo kuanza kutumika rasmi Juni 27, yakilenga kupunguza masharti ya mtu kustahili kupata uraia wa nchi mbili.

Mkuu wa ofisi ya chama kinachowakilisha maslahi ya miji ya Ujerumani, Helmut Dedy aliliambia shirika la habari la DPA kwamba dhamira ilikuwa sio tu kuurahisishia umma kuipata pasipoti hiyo lakini pia kwa uharaka zaidi.

Sheria mpya ya uraia, iliyopitishwa na muungano wa mrengo wa kati wa Kansela Olaf Scholz, kadhalika inatoa fursa ya watu kutuma maombi ya uraia baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka mitano, badala ya mahitaji ya hapo awali ya miaka minane, ili mradi watimize masharti yote.