1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wakiatamili wapigwa marufuku kuingia Umoja wa Ulaya

27 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEX9

Brussels:

Umoja wa ulaya umewapiga marufuku waasi wa Tamil Tiger nchini Sri Lanka kuingia katika nchi yoyote mwanachama. Hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja. Umoja wa ulaya pia umesema unazingatia kuwaingiza waasi hao katika orodha ya makundi ya kigaidi. Katika taarifa umoja huo ulisema umesikitishwa na kuuwawa karibuni kwa Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sri Lanka ambapo serikali imewashutumu waasi wa kundi hilo la Tamil Tiger. Umoja wa ulaya pia umewataka waasi hao waheshimu kikamilifu makubaliano ya kusimamisha mapigano na serikali ya 2002.