1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Tuaregs wafanya uvamizi Niger

Jane Nyingi29 Juni 2007

Nchi ya Niger iliyo miongoni mwa mataifa yanaoongoza duniani katika , uzalishaji wa madini aiana ya uranium inakabiliwa na uasi kutoka kwa watu wa kabila la Tuaregs wenye tabia ya kuhama hama katika jagwa la sahara, japokuwa serikali imekataa katakata kukiri swala hilo.

https://p.dw.com/p/CHkL
Wakaazi wa Niger wakitafakari la kufanya kufuatia uvamizi wa waasi wa Kituaregs
Wakaazi wa Niger wakitafakari la kufanya kufuatia uvamizi wa waasi wa KituaregsPicha: DW / Debrabandère

Nchi ya Niger iliyo miongoni mwa mataifa yanaoongoza duniani katika , uzalishaji wa madini aiana ya uranium inakabiliwa na uasi kutoka kwa watu wa kabila la Tuaregs wenye tabia ya kuhama hama katika jagwa la sahara, japokuwa serikali imekataa katakata kukiri swala hilo.

Mashambulizi hayo hasa yanatekelezwa kaskazini mwa Niger. Rais wa taifa hilo Mamadou Tanja anazielekeza lawama zote kwa makundi ya kigaidi licha ya watu kutoka kabila la Tuaregs kukiri kuhusika.

Shirika la msalaba mwekundu kwa sasa linawapa matibabu wanajeshi 30 waliojeruhiwa, kufuatia uvamizi na kundi hilo katika kampuni mbili zilizochini ya usimamizi wa kijeshi. Wakati wa uvamizi huo wa macheo wanajeshi 15 waliuawa.

Watuaregs hao wanasema uasi huo ni katika kuishinikiza serikali ya Niger kutekeleza makubaliano waliyoafikiana mwaka 1995. Katika makubaliano hayo serikali ya rais Mamadou ilikuwa imewaahidi kuwapa kazi za juu katika kampuni za madini nchini humo.

Jamii hiyo imetengwa katika nchi nyingi wanazoishi, na imekabiliwa na hali ngumu ya maisha ambayo kila kukicha inaeendelea kuzorota kutokana na kufariki kwa mifugo wao. Pigo kubwa lilikuwa mwaka wa 1972 hadi 1974 na pia mwaka wa 1984-1985 wakati kulitokea ukame hali iliyowabadili kuwa watu wa kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Hata hivyo wengine wameamua kujiingiza katika secta ya kilimo huku wengine wakitafuta ajira kwenye sehemu za mijini.

Wengi wanahisi kuwa hatua ya rais Mamadou ya kukataa kuwepo kwa tatizo hilo la wa Tuaregs ni kwasababu ya uhusiano wake wa karibu na kabila hilo.