1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Rwanda wataka paundwe Tume ya kimataifa.

Mohammed Abdulrahman29 Aprili 2005

Wasema ni muhimu kabla ya kuamua kurudi nyumbani kutoka Kongo.

https://p.dw.com/p/CHgz
wahanga wa mauaji ya hailiki nchini Rwanda 1994.
wahanga wa mauaji ya hailiki nchini Rwanda 1994.Picha: AP

Kundi la waasi wa Kihutu nchini Rwanda ambalo mwezi uliopita lilitangaza kwamba litaweka chini silaha bila masharti, na kurudi nyumbani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, sasa wanataka liweko jopo la kimataifa litakalosimamia hatua hiyo.

Waasi wahao wa kundi linalojulikana kama Democratic Forces for t he Liberation of Rwanda-FDLR, wanataka paweko na tume maalum kusimamia hatua ya kuerudi nyumbani baada ya kusalimisha silaha zao, wakisisitiza kwamba tume ya aina hiyo ni muhimu na inahitajika haraka.

Taarifa ya kundi hilo ilisema tume hiyo itakayowajumuisha wajumbe kutoka jumuiya ya kimataifa, serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , serikali ya Rwanda na waakilishi wa kundi hilo, iwe na kazi ya kusimamia mapendekezo yaliotokana na mazungumzo yaliofanyika mjini Roma ambapo waasi hao walitangaza azma hiyo ya kuachana na matumizi ya nguvu.

Taarifa yao kwa hivyo ikasisitiza kwamba amani na demokrasia katika eneo la maziwa makuu inahitaji utekelezaji wa tume hiyo, na kuutaka umoja wa mataifa , umoja wa Afrika na umoja wa ulaya kushiriki.

Wanachama wa kundi hilo ambao wengi wao wanashutumiwa kuhusika na muaji ya halaiki nchini Rwanda 1994, na ni wapinzani wa serikali ya sasa inayoongozwa na Watutsi; wamekua katika misitu ya mashariki mwa Kongo kwa mwaka wa 11 sasa, na kuweko kwao kumezusha mvutano baina ya serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na jirani yake Rwanda.

Lakini machi 31 mwaka huu, kufuatia mazungumzo na serikali ya Kinshasa nchini itali, Viongozi wa kundi hilo la waasi wa Rwanda walitoa taarifa ya kushangaza ambapo mbali na kutambua makosa yaliofanywa wakati wa mauaji hayo, lakini pia wakasema wanasimamisha mapigano na kuwa tayari kurudi nyumbani –Rwanda.

Ahadi hiyo ilikaribishwa na jumuiya ya kimataifa, lakini ikapokelewa kwa shaka shaka na serikali ya Rwanda, imkisema waasi wanaoshutukiwa kuhusika na mauaji lazima wafikishwe mbele ya vyombo vya kisheria kujibu shutuma na mashitaka yanayowakabili.

Mbali na hayo mwezi mmoja baada ya tangazo lao, hadi sasa hakuna mauasi yeyote wa kundi hilo aliyeondoka jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na kurudi Rwanda , huku matukio ya matumizi ya nguvu yakiendelea katika baadhi ya maeneo yaliokaribu na kambi zao.

Kwa upande wake Rwanda jana ilisema iko tayari kuwapokea waasi wa Kihutu watakaorudi nyumbani, lakini ikasisitiza kwamba watakaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya 1994 lazima wafikishwe mahakamani.

Kundi la FDLR- likiwa na wapiganaji baina ya 8,000 na 15,000 liliundwa mwaka 2000 kutokana na wanamgambo wa kihutu Interahamwe na jeshi la zamani la Rwanda, waliohusika katrika mauaji ya karibu watu laki 8-wahutu wa masimamo wa wastani na watutsi walio wachache nchini humo.

Wakati hayo yakiendelea mahakama ya umoja wa mataifa kuhusu mauaji ya Rwanda iliko mjini Arusha Tanzania, ilimhukumu kifungo cha maisha jana afisa mmoja wa zamani wa Kinyarwanda, kwa kuhusika na mauaji na ubakaji . Afisa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 44 Mikaeli Muhimana nayejulikana kwa jina la utani kama-MIKA-, alipatikana na hatia ya kushiriki katika vitendo hivyo katika wilaya ya Kibuye, ambako maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wengi wao watutsi walikimbilia kujinusuru na mauaji. Amepatikana na hatia ya kuwaingilia kwa nguvu wanawake 27 wakitutsi na mauaji ya waafanyabiashara kadhaa wa kitutsi waliokatwa vichwa na sehemu zao za siri . Muhimana alikamatwa nchini Tanzania Novemba 1999 na kesi yake ilianza Machi mwaka jana . Kufuatia hukumu hiyo ya jana , mahakama hiyo ya Arusha sasa imeshawakuta na hatia na huwakumu washtakiwa 22 na kuwaachia huru watu 3.