1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vizuizi dhidi ya wanawake ni uhalifu dhidi ya ubinaadamu

26 Mei 2023

Mashirika ya kimataifa kutetea haki za binaadamu, Amnesty International na International Commission of Jurists, wametoa ripoti inayotaka uchunguzi wa vizuizi vya Taliban dhidi ya haki za wanawake na wasichana Afghanistan

https://p.dw.com/p/4RqZ9
Afghanistan Frauen-Rechte | Demo in Köln
Picha: Ying Tang/NurPhoto/IMAGO

Ripoti hiyo iliyopewa jina "Vita vya Taliban kwa wanawake: Uhalifu dhidi ya ubinaadamu wa unyanyasaji wa kijinsia nchini Afghanistan," iliinukuu sheria ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu,  ICC, inayoorodhesha unyanyasaji wa kijinsia kama uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mataifa yajadili haki za wanawake wa Afghanistan

Ripoti hiyo imelezea juu ya vikwazo vikali vilivyowekwa na Taliban kwa wanawake na wasichana, baada ya kurejea mamlakani Agosti 2021 wakati wanajeshi wa Marekani na NATO kuondoka nchini humo baada ya miongo miwili ya vita.

Ripoti hiyo aidha, imelishutumu Taliban kwa kuwalenga wanawake na wasichana walioandamana kwa amani kwa kuwaweka kizuizini, kuwatowesha kwa nguvu na kuwaweka chini ya ulinzi.