1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Virusi vya Corona vyaanza kuathiri uchumi

29 Februari 2020

Mripuko wa virusi vya Corona Ijumaa hii ulianza kuonekana zaidi kama mgogoro wa kiuchumi duniani kote katika wakati ambapo wasiwasi unaongezeka kufuatia ripoti za maambukizi mapya.

https://p.dw.com/p/3YcpD
Japan Tokio Kursrückgänge an den Börsen
Picha: picture-alliance/Jiji Press/M. Taguchi

Mripuko wa virusi vya Corona Ijumaa hii ulianza kuonekana zaidi kama mgogoro wa kiuchumi duniani kote katika wakati ambapo wasiwasi juu ya maambukizo, ukisababisha kufungwa maduka, kufutwa kwa shughuli mbalimbali pamoja na bustani za kitalii, kusitishwa kwa biashara na usafirishaji lakini pia kuzorotesha zaidi masoko ya fedha ambayo tayari yametikisika.

Waajiri wanaowaambia watumishi kukaa nyumbani wanaongezeka, maakazi kufungwa na hata mshule. Juhudi hizi pana za kuzuia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo zinatishia ajira, malipo na hata faida. Mtaalamu mmoja kutoka taasisi ya Peterson, inayohusika na masomo ya uchumi wa kimataifa Jacob Kirkegaard amesema, "hili ni suala ambalo kiuchumi, suluhu yake ni ngumu kuliko maradhi yenyewe. Amesema unapoyaweka majiji kwenye karantini....unasimamisha shughuli za kiuchumi ambazo huwezi kuzirejesha tena."

Orodha ya mataifa yaliyokumbwa na vorusi hivyo imepanda na kufikia 60, wakati Mexico, Belarus, Lithuania, New Zealand, Nigeria, Azerbaijan, Iceland na Uholanzi yakiripoti visa vya kwanza vya Corona. Zaidi ya watu 83,000 ulimwenguni kotewameambukizwa virusi hivyo huku idadi ya vifo ikifikia 2,800.

Coronavirus Brasilien
Mataifa mbalimbali yameendelea kutangaza kukabiliwa na maradhi ya CoronaPicha: Imago Images

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO Tedros Adhanom Gebreyesus ametangaza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo duniani ilikuwa ya juu sana akiangazia kuendelea kuongezeka kwa idadi ya visa lakini pia mataifa yanayoripoti kuwa na wagonjwa wa Corona.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameziomba serikali "kuchukua hatua zozote zinazowezekana kuudhibiti ugonjwa huo." Maeneo kadha wa kadha ya kiuchumi yalionekana kuanza kuathirika, ikiwa ni pamoja na masoko ya hisa kama Wall Street la nchini Marekani.

Huko Asia, eneo la michezo na la kitalii maarufu Disneyland pamoja na studio za kurekodi filamu za Universal nchini Japan wametangaza kufunga na shughuli zilizotarajiwa kuwavutia makumi kwa maelfu ya watu zimeahirishwa. Lakini pia maafisa wa Japan wanajiandaa kufunga shule hadi mapema mwezi Aprili. 

Nchini Italia, kumeripotiwa visa 888. Italia ni taifa lililoathirika zaidi nje ya bara la Asia.Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte alionyesha dhahiri wasiwasi wa kudorora kwa uchumi.

Serikali ya Uswisi imezuia matamasha ya watu zaidi ya 1,000. Kwenye ripoti iliyochapishwa hapo jana kwenye jarida la tiba la New England, maafisa wanasema kiwango cha vifo kutokana ugonjwa huo ilikuwa asilimia 1.4, wakizingatia wagonjwa 1,099 waliopo zaidi ya hospitali 500 kote nchini China.

Washington US Präsident Donald Trump
Rais Donald Trumo wa Marekani hataweza kukutana na viongozi wa ASEAN kutokana na kitisho cha CoronaPicha: picture-alliance/newscom/T. Katopodis

Marekani imesitisha mkutano na viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la Kusinimashariki mwa Asia, ASEANMataifa ya ASEAN yaunda rasmi jumuiyauliopangwa kufanyika machi 14, kutokana na wasiwasi kuhusu mripuko huo wa Corona, maafisa wawili wa Marekani wenye ufahamu kuhusu mkutano huo wamesema jana Ijumaa. 

Rais Donald Trump aliwaalika viongozi hao wa mataifa 10 wanachama wa ASEAN kukutana naye jijini Las Vegas baada ya kushindwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi hilo mjini Bangkok, mwezi Novemna mwaka jana.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametaka juhudi madhubuti zaidi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, akisema kutakuwa na athari mbaya sana iwapo ugonjwa huo utaingia nchini mwake.

Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini limesema kwamba Kim ameiagiza ofisi kuu ya kitaifa ya mapambano dhidi ya majanga kuimarisha uchunguzi na vipimo ili kufunga njia zote zinazoweza kutoa njia kwa virusi hivyo kuingia nchini humo.

Mashirika: ape/rtre