1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Viongozi wa Sudan Kusini na Afrika Kusini wafanya mazungumzo

28 Juni 2023

Rais wa Sudan Kusini amefanya mazungumzo mjini Pretoria na mwenzake wa Afrika Kusini kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Sudan na mchakato dhaifu wa amani mjini Juba.

https://p.dw.com/p/4TBZd
Salva Kiir Mayardit | sudanesischer Präsident
Rais wa Sudan Kusini Salva KiirPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Marais Salva Kiir na Cyril Ramaphosa walitarajiwa kuyajadili masuala yanayowahusu pamoja na vita vinavyoendelea Sudan.

Taarifa ya ofisi ya Rais wa Afrika Kusini imesema viongozi hao wawili pia walitarajiwa kutathmini hatua zilizopigwa kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini.

Mzozo unaoendelea Sudan, jirani ya Sudan Kusini katika upande wa kaskazini, umesababisha zaidi ya Wasudan Kusini 100,000 kurejea makwao.

Umoja wa Mataifa umesema mmiminiko huo umezusha wasiwasi wa kutokea machafuko mapya ya kikabila.

Watu 13 waliuawa katika kambi ya ulinzi wa raia mapema mwezi huu.

Wakati huo huo, majenerali wawili wanaowania madaraka nchini Sudan, wametangaza usitishaji mapigano ili kupisha maadhimisho ya Sikukuu ya Eid Al Adh'ha yanayofanyika leo.