1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais wa Afrika Kusini na ujumbe wake wa Afrika wako Urusi

17 Juni 2023

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewasili mjini Saint Petersburg, Urusi tayari kwa mazungumzo na rais Vladimir Putin, yanayoongozwa na ujumbe wa Afrika ya kushinikiza makubaliano kati ya Kyiv na Moscow

https://p.dw.com/p/4SihJ
Russland | Südafrikas Präsident Cyril Ramaphosa in St Petesburg
Picha: Grigory Sysoyev/AFP

Ramaphosa amewasili Saint Petersburg baada ya mazungumzo na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wa Ukraine, na ujumbe wake unajumuisha marais wanne ambao ni pamoja na Macky Sall wa Senegal, Hakainde Hichilema wa Zambia na Azali Assoumani wa Comoro ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Soma pia: Ujumbe wa viongozi wa Afrika kukutana na rais Putin wa Urusi

Baada ya mazungumzo na Zelensky, Ramaphosa alitoa mwito wa amani kwa njia ya mazungumzo, ingawa Zelensky aliondoa uwezekano huo.

Ujumbe huu unafanya ziara wakati mataifa hayo mawili yakijikita katika kuimarisha mashambulizi, na Kyiv ikiongeza mashambulizi yake mapya ya kushtukiza.