1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya China na bara la Afrika kufanyika wiki hii.

Josephat Charo
2 Septemba 2024

China inatarajia kuzipa nchi za Afrika mikopo zaidi kuziwezesha kufanya miradi mikubwa mikubwa ya maendeleo.

https://p.dw.com/p/4kA95
Mkutano wa ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAS) 20!8
Mkutano wa ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAS) 20!8Picha: Li Tao/Photoshot/picture alliance

Viongozi wa nchi za Afrika wanasafiri kwenda Beijing wiki hii kutafuta fedha kwa ajili ya kufadhili miradi mikubwa wakati wanapopania ushindani wa mamlaka makubwa unaoendelea kuongezeka kuhusu raslimali na ushawishi barani Afrika.

China imesema mkutano kati yake na nchi za Afrika wiki hii utakuwa tukio kubwa la kidiplomasia tangu janga la corona, huku viongozi wa Afrika Kusini, Nigeria, Kenya na mataifa mengine wakithibitisha watahudhuria na wajumbe wengine kadhaa wakitarajiwa.

China imetanua mahusiano na nchi za Afrika katika muongo mmoja uliopita, ikizipatia mabilioni ya mikopo ambayo imesaidia kujenga miundombinu, lakini wakati mwingine imezipa nchi hizo mizigo mikubwa ya madeni.