1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini na Japan zajadili kuboresha uhusiano wao

7 Mei 2023

Viongozi wa Korea Kusini na Japan, wamefanya mazungumzo juu ya kushughulikia mivutano ya kihistoria kati ya nchi hizo na changamoto zinazotokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4R0Sc
Südkorea Seoul | Besuch Premierminister Kishida Japan
Picha: Chung Sung-Jun/Getty/AP/picture alliance

Viongozi wa Korea Kusini na Japan, katika muda usiozidi miezi miwili wamekutana leo kwa kikao cha pili cha mazungumzo juu ya kushughulikia mivutano ya kihistoria kati ya nchi hizo vilevile kuboresha uhusiano wao na kuzikabili changamoto zinazotokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Na kwa ajili hiyo waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida anafanya ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini baada ya mwenzake wa Korea Kusini rais Yoon Suk Yeol kufanya ziara nchini Japan mnamo mwezi Machi. Vyombo vya habari vya Korea Kusini vinasubiri kuona iwapo waziri mkuu wa Japan ataomba radhi kwa uwazi zaidi juu ya udhalimu wa ukoloni wa Japan nchini Korea Kusini kuanzia mwaka 1910 hadi mwaka 1945.