1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G7 kujadili uhamiaji, Afrika na akili mnemba

14 Juni 2024

Viongozi wakuu wa mataifa ya G7 wanatarajiwa kujadili changamoto kadhaa zinazoikabili dunia katika siku ya pili ya mkutano wao wa kilele unaofanyika nchini Italia.

https://p.dw.com/p/4h2Mt
Italia
Mkutano wa G7 wafanyika Italia Picha: Nicholas Berardo

Mada zitakazojadiliwa hii leo ni pamoja na uhamiaji, kanda ya Indo-Pasifiki na usalama wa kiuchumi Afrika na teknolojia ya akili ya kubuni miongoni mwa nyingine. 

Viongozi hao pia wanatarajiwa kuelezea wasiwasi kuhusu uwezo wa kiviwanda wa China uliopitiliza na uungwaji wake mkono kwa Urusi. 

Biden, Zelensky wasaini mkataba wa ´kihistoria´ wa usalama

Kiongozi  mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis atahudhuria kikao cha leo ambapo atatoa hotuba kuhusu hatari na uwezo wa teknolojia ya akili ya kubuni. 

Viongozi kadhaa kutoka mataifa yasio wanachama wa G7 watahudhuria mkutano huo, wakiwemo waziri mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Kenyan William Ruto, miongoni mwa wengine.