1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden, Zelensky wasaini mkataba wa ´kihistoria´ wa usalama

14 Juni 2024

Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky jana Alhamisi wametia saini mkataba wa usalama wa miaka 10 baina ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4h15W
Rais Joe Biden wa Marekani (kulia) na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais Joe Biden wa Marekani (kulia) na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Picha: Presidential Office of Ukraine/ZUMA Press Wire/picture alliance

Mkataba huo utakashuhudia Washington ikiupatia utawala mjini Kyiv msaada wa kijeshi na mafunzo kwa muongo mmoja unaokuja.

Halfa ya utiaji saini mkataba huo imefanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa kundi la mataifa tajiri duniani la G7 uliofunguliwa jana kwenye mkoa wa mwambao wa Italia wa Apulia.

Zelensky ameitaja siku ya utiaji saini mkataba huo kuwa ya kihistoria katika mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi na kwamba anatumai mafunzo na msaada wa kijeshi wa Marekani utafungua njia kwa hatimaye Ukraine kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Kwa upande wake Rais Biden amesema mataifa ya kundi la G7 yamechukua hatua madhubuti kumwonyesha Rais Vladimir Putin wa Urusi kwamba hatoweza kuushinda mshikamano wa wanademokrasia.