1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Viongozi wa EAC wakutana kujadili mzozo wa Kongo

4 Februari 2023

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo nchini Burundi kwa mkutano wa kilele juu ya mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4N68G
Ruandas Präsident Paul Kagame Felix und DR Kongos Präsident Tshisekedi
Picha: Simon Wohlfahrt/AFP

Ofisi ya chombo hicho cha kikanda kinachoongoza juhudi za kumaliza machafuko nchini Kongo imeandika kwenye ukurasa wa Twitter kuwa ajenda ya mkutano huo wa leo itakuwa ni kutathmini hali ya usalama mashariki mwa Kongo na hatua zinazofuata. Ofisi ya rais wa Kongo imesema rais Felix Tshisekedi atahudhuria mazungumzo hayo.

Hata hivyo haijafahamika iwapo viongozi wengine wa kanda hiyo yenye mataifa 7 wanachama watasafiri kwenda Burundi kwa mutano huo. Wiki iliyopita, Qatar ilikuwa imepanga kuandaa mkutano kati ya Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame, lakini wanadiplomasia wakasema kiongozi huyo wa Kongo alikataa kuhudhuria.