1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Afrika kutatua mzozo wa Ukraine

17 Mei 2023

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema viongozi sita wa Afrika wanapanga kwenda Urusi na Ukraine haraka iwezekanavyo kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa suluhu la vita vinavyoendelea baina ya mataifa hayo mawili

https://p.dw.com/p/4RUXD
BRICS Treffen in Brasilien/Vladimir Putin und Cyril Ramaphosa
Picha: Mikhail Metzel/ITAR-TASS/IMAGO

Rais Ramaphosa amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky  wameridhia kupokea ujumbe na wakuu wa nchi za Afrika mjini huko Moscow na Kyiv. Mwishoni mwa juma lililopita Ramaphosa alielezwa kufanya mazungumzo kwa njia ya simu kwa nyakati na Rais Putin na kadhalika Rais Zelensky, ambapo aliwasilisha jitihada iliyoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Zambia, Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Misri na taifa lake Afrika Kusini.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Cape Town, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu wa Singapore, Lee Hsien Loong. Ramaphosa amesema amekubaliana na pande hizo  hasimu  kuanza maandalizi ya mazungumzo na viongozi wa Afrika na kwamba anatarajia kufanyika makubaliano ya kina. "Majadiliano yangu na viongozi hao wawili yalionyesha kuwa wote wako tayari kupokea viongozi wa Afrika na kuwa na majadiliano juu ya jinsi mzozo huu unaweza kumalizwa. Ikiwa hilo litafaulu au la itategemea majadiliano yatakayofanywa,"alisema Ramaphosa

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika unataarifa

Themenpaket - Ukraine - Zerstörung - Minenräumung - Europa-Rat Gipfel in Reykjavik
Mji wa Mykolaiv wa UkrainePicha: Vincenzo Circosta/Zumapress/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na Umoja wa Afrika wamepewa taarifa kuhusu mpango huo. Hata Ramaphosa hakutoa ratiba maalum ya ziara hiyo au maelezo mengine ya ziada , lakini amesema tu kwamba mzozo wa Urusi na Ukraine umekuwa wa kuangamiza na Afrika pia inateseka sana kutokana na vita hiyo.

Nchi za Afrika zimeathiriwa vibaya na kupanda kwa bei ya nafaka na athari kwa biashara ya dunia. Tangazo limetolewa siku moja baada ya Ramaphosa kusema Afrika Kusini imekuwa katika shikikiza kubwa la kuchagua upande katika mzozo huo, kufuatia shutuma kutoka kwa Marekani kwamba Pretoria inaipa silaha kwa serikali ya Moscow hatua ambayo ingevunja ahadi yake kutoegemea upande wowote.

Majeshi ya Ukraine yawafarushwa wa Urusi kandoni mwa Bakhmut

Ndani nchini Ukraine, Serikali ya taifa hilo imesema imefanikiwa kuvirudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka pembezoni mwa mji unaogombaniwa wa Bakhmut lakini pia imekiri kwamba vikosi vya Moscow vilikuwa vinaingia ndani zaidi ndani ya mji huo uliovurugwa kwa vita.

Soma zaidi:Urusi: Ukraine imetumia makombora ya Uingereza kuwalenga raia

Tangazo hilo limetolewa wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisema viongozi wa Ulaya wanaokutana nchini Iceland wamekikubaliana kuunda kile walichokiita "orodha la uharibifu" ili kurekodi madhara na uharibifu wa wakati wa vita uliofanywa na Urusi nchini Ukraine. Mwaka mmoja baada ya kuiondoa Urusi katika Baraza la Ulaya (CoE) kutokana na vita vyake nchini Ukraine, viongozi wa  baraza hilo lenye mataifa 46 wanakutana mjini Reykjavik, ajenda kuu ikiwa mzozo wa Ukraine.

Chanzo: AFP

Mhariri: Daniel Gakuba