1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIKWAZO DHIDI YA LIBERIA VIBAKIE:

23 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFq0

MONROVIA: Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia Jacques Klein amesema vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo vinapaswa kubakia.Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa akaongezea kuwa ingawa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesita,serikali ya Liberia na uchumi wa nchi hiyo ungali katika hali ya vurugu.Kabla ya kuviondosha vikwazo hivyo,Umoja wa Mataifa lazima uhakikishe kuwa rasli mali ya taifa inatumiwa kwa manufaa ya wananchi wake.