1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza operesheni ya kijeshi Ukingo wa Magharibi.

4 Julai 2023

Operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel katika Ukingo wa Magharibi inaendelea kwa siku ya pili. Wapalestina wasiopungua 10 wameuawa na maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4TODu
Israeli forces strike West Bank city
Picha: Mohamad Torokman/REUTERS

Wanajeshi wa Israel wamesonga mbele na msako wa wapiganaji wa kipalestina kwenye kambi iliyopo katika Ukingo wa Magharibi. Ikiwa ni siku ya pili tangu msako huo uanze wapalestina 10  wameshauawa na maalfu wamekimbia na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa.

Majeshi ya Israel yafanya operesheni katika mji wa Jenin ulio katika Ukingo wa Magharibi.
Majeshi ya Israel yafanya operesheni katika mji wa Jenin ulio katika Ukingo wa Magharibi.Picha: Raneen Sawafta/REUTERS

Wizara ya afya ya Palestina imesema 20 kati ya watu hao waliojeruhiwa wako katika hali mbaya. Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amelaani operesheni hiyo ambayo ameiita kuwa ni uhalifu mpya wa kivita.

Soma:Wahanga wa operesheni ya kijeshi ya Israel Jenin wafikia 10

Mamlaka ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi nan chi tatu za kiarabu zilizo na uhusiano na Israeli ambazo ni Jordan, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu na Jumuiya ya Nchi 57 za Ushirikiano wa Kiislamu zimelaani mashambulizi hayo ya Israel.

Mara baada ya operesheni kuanza utawala wa Palestina unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ulitangaza kusimamisha mawasiliano na Israel hatua iliyozua wasiwasi kwa Marekani na kwenye Umoja wa Mataifa.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Wanajeshi wa Israel wanaendesha operesheni hiyo wakati ambapo waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu yuko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wake wa kisiasa wa vyama vya mrengo mkali. Vyama hivyo vinamtaka Netanyahu achukue msimamo mkali kujibu mashambulio ya hivi karibuni yaliyofanywa dhidi ya walowezi wa kiyahudi, ikiwa pamoja na kuuliwa kwa walowezi wanne.

Soma:Israel yafanya operesheni kubwa ya kijeshi mjini Jenin

Moshi mzito ulionekana mara kwa mara juu ya kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, mji ambao kwa muda mrefu umekuwa kambi muhimu ya wapiganaji wa kipalestina. Jeshi la Israel lilisema Jumatatu kuwa operesheni yake ni kwa ajili kulenga baadhi ya maeneo katika mji wa Jenin kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwa ni sehemu ya juhudi zake kubwa za kukabiliana na ugaidi likiwemo eneo moja ndani ya kambi ya wakimbizi iliyo kando ya mji huo wa Jenin ambalo jeshi la Israel limesema lilikuwa linatumiwa na wapiganaji na wanamgambo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Picha: Alberto Pezzali/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Israel,admeli Daniel Hagari ameeleza kuwa Israel imeanzisha operesheni hiyo, kwa sababu mashambulio yapatayo 50 mnamo kipindi cha mwaka uliopita yalitokea kwenye mji wa Jenin.

Vyanzo:AP/DPA/RTRE/AFP