1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Iran kutowa mapendekezo kwa mazungumzo ya nuklea

27 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhJ

Mjumbe mpya wa msimamo mkali wa Iran katika mazungumzo ya suala la nukela Ali Larijani amesema serikali ya Iran inapanga kutowa mapendekezo mapya kuhusu mazungumzo hayo na Umoja wa Ulaya katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

Taarifa yake inafuatia mkutano wake na kiongozi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Mohammed El Baradei mjini Vienna.Imesema Iran haikufuta uwezekano wa kuwa na majadiliano zaidi na Umoja wa Ulaya juu ya kwamba Umoja wa Ulaya umevunja mazungumzo hayo kupinga Iran kuanza tena shughuli zake za kurutubisha nishati ya nuklea.

Larijani hata hivyo ameongeza kusema kwamba tishio la uwezekano wa kuwekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana mpango wake huo wa nuklea halikuifanya serikali yake kuwa na wasi wasi.