1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Bei ya mafuta ghafi yapindukia dola 57 kwa pipa

18 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVz

Bei za mafuta ghafi zimepanda kufikia rekodi mpya ya juu ya zaidi ya dola 57 kwa pipa.

Kupanda huko kwa bei kumekuja baada ya Umoja wa Nchi zenye kusafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC kuamuwa kuongeza uzalishaji kwa mapipa 500,000 kwa siku kukidhi mahitaji ya dunia yanayozidi kuongezeka.

Wakati huo huo Marekani imeidhinisha mpango wa kuchimba mafuta na gesi katika Hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori ya Arctic.Akiitetea hatua hiyo inayopingwa na wanamazingira Rais George W Bush amesema itaufanya uchumi wa Marekani usitegemee sana mafuta yanayoagiziwa kutoka Mashariki ya Kati.