1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Vibanda vya kupigia kura vya chomwa moto Bangladesh

6 Januari 2024

Watu wasiojulikana wamezichoma moto shule tano za msingi ikiwa ni pamoja na vibanda vinne vya kupigia kura nchini Bangladesh.

https://p.dw.com/p/4avKS
Uchaguzi mkuu wa Bangladesh kuitishwa Jumapili huku chama kikuu cha upinzani kimetangaza kuususia
Uchaguzi mkuu wa Bangladesh kuitishwa Jumapili huku chama kikuu cha upinzani kimetangaza kuususiaPicha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Polisi imesema inachunguza mkasa huo uliotokea kwenye kitongoji cha Gazipur nje kidogo ya mji mkuu Dhaka lakini pia inashuku watu waliohusika wanalenga kuvuruga uchaguzi utakaofanyika kesho Jumapili kwa kuzusha hofu na kuharibu miundombinu ya kupigia kura.

Hayo yameripotiwa katika wakati chama kikuu cha upinzani cha Bangladesh Nationalist (BNP), kinasusia uchaguzi mkuu wa kesho ikiwa ni mara ya pili katika chaguzi tatu zilizopita nchini Bangladesh.

Wamewataka wapiga kura kutokwenda vituoni na kufanya mgomo wa siku mbili kuonesha hasira dhidi ya kile wamekitaja kuwa matayarisho mabovu ya uchaguzi huo unaotarajiwa kumpa ushindi waziri mkuu Sheikh Hasina.