1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaitaka Bangladesh kumwachia kiongozi wa upinzani

8 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Bangladesh kumwachilia huru kiongozi mkuu wa chama cha upinzani ili aweze kutibiwa.

https://p.dw.com/p/4YYDf
Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk.
Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk.Picha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amemtaka Waziri Mkuu wa BangladeshSheikh Hasina kumwachilia huru kiongozi mkuu wa chama cha upinzani BNP, Khaleda Zia ili aweze kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya haraka.

Baada ya serikali ya Hasina kukataa ombi la kumruhusu kuondoka nchini humo, madaktari wa Bangladesh wamesema Zia (78), aliyekuwa waziri mkuu mara mbili, yupo katika "hatari kubwa" ya kufa ikiwa hatopewa matibabu nje ya nchi. 

Soma pia:Polisi Bangladesh inamshikilia kiongozi wa upinzani huku kukiwa namaandamano dhidi ya serikali

Turk amesema kuachiwa kwa Zia itakuwa ni hatua muhimu kuelekea mazungumzo ya kisiasa na maridhiano.

Khaleda Zia amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 17 jela mwaka 2020.

Hasina na Zia wamekuwa wapinzani wakuu kwa zaidi ya miongo minne katika siasa za taifa hilo la Asia Kusini lenye wakazi wapatao milioni 170.