1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yashambulia miundo mbinu ya nishati Syria

11 Oktoba 2023

Mashambulizi ya mabomu ya Uturuki yamesababisha uharibifu wa zaidi ya nusu ya miundo msingi ya umeme na mafuta katika eneo la kaskazini mashariki la Syria linaloshikiliwa na wanamgambo wa Kikurdi.

https://p.dw.com/p/4XPyR
Moto uliosababishwa na mlipuko Syria
Moto uliosababishwa na mlipuko SyriaPicha: picture-alliance/Xinhua News Agency/A. Safarjalani

Kulingana na kamanda mkuu wa wanamgambo hao Mazloum Abdi ambaye anaongoza kikosi cha jeshi cha SyrianDemocratic Forces kinachoungwa mkono na Marekani, mashambulizi hayo ni pigo kwa uchumi wake unaotegemea nishati.

Katika mahojiano na shirika la habari la Ufaransa AFP, Abdi vile vile ameikosoa Marekani kwa kutochukua hatua zaidi kuzuia mashambulizi hayo.

Soma pia:Syria yafanya maziko ya wahanga wa shambulizi la droni

Mnamo Oktoba 5, Uturuki ilianzisha mashambulizi ya mabomu kaskazini mashariki mwa Syria baada ya kusema kwamba wanamgambo waliofanya shambulizi mjini Ankara walitokea na kupewa mafunzo yao nchini Syria.