1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake ni wachache katika nafasi za juu Ujerumani

17 Januari 2024

Idadi ya wanawake wanaoshikilia nyadhifa za juu katika kampuni kubwa za Ujerumani inapungua. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya DIW ambao unachora picha mbaya kwa uongozi wa Olaf Scholz

https://p.dw.com/p/4bNim
Ujerumani | Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Jens Krick/Flashpic/picture alliance /

Taasisi hiyo ya utafiti ya DIW imesema kuwa, maafisa wakuu watendaji wanawake katika makampuni makubwa 200 ya Ujerumani walikuwa tisa pekee mwishoni mwa mwaka 2023, idadi hiyo ikiwa chini tofauti na mwaka 2022 ambapo kulikuwepo na maafisa 10 wakuu watendaji wanawake. Mwaka 2021, idadi hiyo ilikuwa ni 14.

Virginia Sondergeld, mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo amesema wanaume wengi ndio wanaoshikilia nafasi za juu kwenye makampuni makubwa ya Ujerumani.

Utafiti huo umebaini kuwa, asilimia 44 ya kampuni hazina wanawake kwenye bodi zao za usimamizi, huku asilimia 40 zikiwa na mwanamke mmoja tu na asilimia 16 ya kampuni hizo zina wanawake wawili tu au zaidi.