1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Usalama wazidi kuzorota nchini Sudan

31 Mei 2023

Mapigano yamezuka upya nchini Sudan licha ya makubaliano ya hivi karibuni ya pande zinazohasimiana ya kusitisha vita.

https://p.dw.com/p/4S0Bw
Mkuu wa majeshi ya Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akizungumza na wanajeshi wake juu ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano.
Majenerali wawili nchini Sudan wameliingiza taifa hilo kwenye mapigano yanayosababisha hali mbaya ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.Picha: Sudanese Armed Forces/REUTERS

Wapatanishi wa Marekani na Saudi Arabia walisema mnamo siku ya Jumatatu kwamba kikosi cha msaada wa dharura RSF na jeshi wamekubali kurefusha mkataba wa kusitisha mapigano kwa siku tano zaidi. Hata hivyo licha ya tangazo hilo, wakaazi wameripoti kutokea kwa mapigano kusini mwa mji mkuu Khartoum na Nyala ambao ni mji mkuu wa jimbo la Darfur kusini. Jana Jumanne, wakaazi waliliambia shirika la habari la AFP kuwa mashambulizi ya anga na mapigano yaliripotiwa kuendelea hadi nyakati za usiku mjini Khartoum na Darfur. Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al- Burham amesema jeshi lake liko tayari kupigana hadi lipate ushindi.