1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mkataba wa usitishaji mapigano Sudan warefushwa kwa siku 5

30 Mei 2023

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema pande zinazohasimiana nchini Sudan zimekubali kuongeza muda wa siku tano zaidi wa kusitisha mapigano, saa chache tu kabla ya kukamilika kwa muda wa mwisho wa mkataba wa awali.

https://p.dw.com/p/4RxOK
Sudan, Khartoum | Anhaltende Kämpfe
Picha: AFP via Getty Images

Saudi Arabia na Marekani ambazo ni wapatanishi katika mzozo wa Sudan kati ya jeshi na kikosi cha msaada wa dharura RSF zimekaribisha makubaliano hayo mapya ya kuongeza muda wa usitishaji mapigano.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeendelea kueleza kwamba, kurefushwa kwa muda huo kutatoa fursa ya usafirishaji wa misaada ya kibinadamu, kuregeshwa kwa huduma muhimu na nafasi ya kufanyika mazungumzo juu ya suluhisho la muda mrefu kuhusu mzozo huo.

Licha ya makubaliano hayo ya kusitisha mapigano kutozingatiwa kikamilifu, takriban Wasudan milioni mbili  wamepokea misaada ya kibinadamu  katika siku za hivi karibuni.