1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yathibitisha kupoteza jenerali wake Ukraine

4 Desemba 2023

Maafisa wa Urusi wamethibitisha kuuliwa kwa jenerali wao katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ZlF1
Urusi imekiri kupoteza jenerali wake mwengine kwenye vita vyake nchini Ukraine.
Urusi imekiri kupoteza jenerali wake mwengine kwenye vita vyake nchini Ukraine.Picha: Marek M. Berezowski/Anadolu/picture alliance

Jenerali Vladimir Zavadsky, ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha Bahari ya Kaskazini, aliuawa wakati wa operesheni maalumu kwenye jimbo la Voronezh linalopakana na Ukraine.

Vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti juu ya kuuwawa kamanda huyo wiki iliyopita.

Soma zaidi: NATO yazidi kuiunga mkono Ukraine

Urusi ilisema majenerali wake sita wameshauliwa katika vita vya Ukraine, lakini Ukraine inadai kwamba majenerali wa Urusi wapatao 12 wameshauawa mpaka sasa.