1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema nchi za Ulaya zitalipa zaidi mahitaji ya gesi

28 Agosti 2024

Urusi imesema nchi za Ulaya zitalipa zaidi kwa ajili ya mahitaji ya gesi ikiwa Ukraine haitarefusha mkataba na Urusi wa kupitishia gesi hiyo ambao unafikia mwisho wake tarehe 31 mwezi Desemba.

https://p.dw.com/p/4k1P6
Mabomba ya gesi
Mabomba ya gesi Picha: ANP/IMAGO

Urusi imesema nchi za Ulaya zitalipa zaidi kwa ajili ya mahitaji ya gesi ikiwa Ukraine haitarefusha mkataba na Urusi wa kupitishia gesi hiyo ambao unafikia mwisho wake tarehe 31 mwezi Desemba.

Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov, amewaambia waandishi habari kwamba Urusi inazo njia nyingine na kwamba maamuzi ya Ukraine yanaweza kuathiri maslahi ya wanunuzi wa barani Ulaya na hasa wale wanaotaka kupata gesi kwa uhakika na kwa bei nafuu.

Hata hivyo, nchi nyingi za Ulaya zinazopata gesi kutoka Urusi zimekuwa zikijitayarisha kuona mwisho wa kupatikana gesi hiyo kutoka Urusi kupitia Ukraine mkataba utakapofikia mwisho. Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya umeiomba Azerbaijan isaidie kuwezesha kufanyika mazungumzo na Urusi juu ya mkataba huo wa kupitishia gesi.