1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaitahadharisha Ukraine kuhusu kuishambulia Crimea

20 Juni 2023

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema wana taarifa kwamba Ukraine inapanga kulishambulia eneo la Crimea.

https://p.dw.com/p/4SqTf
Yevpatoria, Russia in pictures
Picha: Alexei Pavlishak/TASS/dpa/picture alliance

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema wana taarifa kwamba Ukraine inapanga kulishambulia eneo la Crimea kwa kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotengenezwa Marekani na Uingereza.

Shoigu ametahadharisha kwamba Urusi itachukua hatua za kulipiza kisasi iwapo Crimea itashambuliwa. Urusi ililitwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine mnamo 2014 lakini inalichukulia kuwa eneo lilo nje ya operesheni ya kijeshi inayolenga mashariki na kusini mwa Ukraine.

Ukraine inapambana kuyakomboa maeneo yake mashariki na kusini mwa nchi huku ikisema imevikomboa vijiji vinane katika awamu ya awali ya operesheni dhidi ya vikosi vya Urusi. Maafisa wa Ukraine wameapa kupata ushindi mkubwa licha ya upinzani mkali kutoka kwa vikosi vya Urusi.