1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wauawa karibu na mpaka wa magharibi mwa Urusi.

30 Aprili 2023

Gavana wa jimbo la Bryansk magharibi mwa Urusi amesema mashambulizi ya leo alfajiri yaliyofanywa na majeshi ya Ukraine katika kijiji cha mpakani cha Suzemka yamesababisha kuuawa watu wanne na wengine wawili wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4QjMy
29/04/2023**Ukraine Raketenangriff Uman
Picha: Carlos Barria/REUTERS

Gavana wa jimbo la Bryansk magharibi mwa Urusi amesema mashambulizi ya leo alfajiri yaliyofanywa na majeshi ya Ukraine katika kijiji cha mpakani cha Suzemka yamesababisha kuuawa watu wanne na wengine wawili wamejeruhiwa. Inashukiwa kijiji hicho kilicho umbali wa kilomita 12 kutoka kwenye mpaka kati ya Urusi na Ukraine, kilishambuliwa usiku wa kuamkia leo kwa ndege isiyokuwa na rubani ambayo ilipiga ghala la mafuta katika rasi ya Crimea inayodhibitiwa na Urusi. Gavana wa jimbo hilo la mpakani amesema hali ya hatari imetangazwa kwenye eneo hilo.Vijiji vya Urusi vinavyopakana na Ukraine katika mikoa ya Bryansk na Belgorod vimekumbwa na mashambulio kadhaa tangu kuanza kea uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.