1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Urusi yaionya Marekani kuachana na mipango yake ya silaha

27 Mei 2023

Urusi hii leo imepuuzilia mbali ukosoaji wa rais Joe Biden wa Marekani kuhusiana na mpango wa Moscow wa kupeleka silaha za nyuklia nchini Belarus.

https://p.dw.com/p/4Rt9y
Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Alexander Lukashenko wa Belarus wakipeana mikono walipokutana kabla ya Gwaride la Ushindi mjini Moscow, Mei 9, 2023.
Urusi na Belarus wamekubaliana upelekwaji wa silaha za nyuklia za kimkakati nchini Belarus, hatua iliyoibua wasiwasi miongoni mwa mataifa ya magharibi.Picha: Vladimir Smirnov/TASS/dpa/picture alliance

Urusi imeionya  Washington na kuongeza kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikipeleka silaha kama hizo barani Ulaya.

Biden amesema mapema leo kwamba amechukizwa sana na ripoti kwamba Urusi imeamua kuendelea na mpango wake wa kupeleka silaha hizo za nyuklia za kimkakati nchini Belarus, baada ya wizara ya mambo ya nje kuulaani mpango huo.

Urusi imesema wana haki na uhuru wa kuhakikisha usalama kwa namna wanayoona inafaa katikati ya vita vilivyoanzishwa na Washington dhidi yao na kuongeza kuwa hatua wanazozichukua zinaendana na wajibu na sheria za kimataifa.

Marekani imesema dunia inakabiliwa na kitisho kikubwa kabisa cha kinyuklia, tangu kile cha Cuba cha mwaka 1962 kutokana na matamshi ya rais Vladimir Putin juu ya mzozo wa Ukraine, lakini Moscow inasema msimamo wake umetafsiriwa vibaya.

Soma Zaidi: Belarus yasema shinikizo la Magharibi limefanya ipokee silaha za nyuklia