1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shinikizo la Magharibi yatufanya tupokee nyuklia - Belarus

28 Machi 2023

Belarus imesema imelazimika kupokea silaha za nyuklia kutoka Urusi kutokana na shinikizo lisilo mfano kutoka nchi za Magharibi.

https://p.dw.com/p/4POXT
Putin und Lukaschenko | Archivbild 2019
Picha: Sergei Chirikov/POOL EPA/AP/dpa/picture alliance

Nchi hiyo imesisitiza kuwa hatua yake hiyo haijakiuka makubaliano ya kimataifa na imechukuliwa kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa kiusalama na kiulinzi. 

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Belarus imeongeza kusema kwamba nchi hiyo imeshuhudia ikiandamwa na shinikizo la kisiasa na kiuchumi kutoka Marekani na washirika wake.

Soma zaidi: NATO yakemea matamshi ya Urusi kuhusu Nyuklia

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephanie Dujarric, ametahadharisha juu ya kuchukuliwa hatua zinazoweza kusababisha janga kufuatia hatua ya Belarus.

Belarus Präsident Alexander Lukaschenko
Rais Alexander Lukaschenko wa BelarusPicha: Vladimir Astapkovich/Kremlin/SPUTNIK/REUTERS

''Ninachotaka kusisitiza kuhusu msimamo wetu juu ya ripoti tulizoziona kuhusu silaha za Nyuklia na Belarus ni kwamba kitisho kilichopo sasa ni kikubwa. Na hatua zote zinazoweza kusababisha makosa au kuongeza mgogoro kwa kusababisha athari kubwa  zinapaswa kuepukwa.'' Alisema.

Soma zaidi: Jumuiya ya kimataifa yakemea mpango wa nyuklia wa Putin

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amesema Belarus itakabiliwa na vikwazo zaidi kufuatia mpango huo wa Urusi wa kuweka silaha za nyuklia katika ardhi ya taifa hilo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW