1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine

1 Juni 2024

Urusi kwa mara nyingine imefanya mashambulizi makali ndani ya ardhi ya Ukraine usiku wa kuamkia leo kwa kuvurumisha makombora na kutuma makumi ya droni kwa sehemu kubwa, ikiilenga miundombinu ya umeme.

https://p.dw.com/p/4gWia
Ukraine
Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine Picha: Artur Abramiv/Zuma/picture alliance

Vituo vya umeme kwenye mikoa mitano ikiwemo Dnipro-petrovsk, Donetsk na Zapo-rizh-zhya  vimeshambuliwa. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati wa nchi hiyo German Galushchenko. 

Kwenye mji mdogo uliopo katika mkoa wa Kharkiv, watu 12 wamejeruhiwa baada ya majengo ya makaazi kushambuliwa kwa makombora. 

Marekani yaidhinisha Ukraine itumie silaha kuyashambulia maeneo ya Urusi

Kulingana na jeshi la anga la Ukraine, Urusi ilirusha makombora 53 ya masafa pamoja na droni 47. Ukraine imesema imefanikiwa kudungua makombora 34 na droni 46.

Hayo yanajiri katika wakati Rais Volodomyr Zelensky wa nchi hiyo anafanya safari mjini Singapore kusaka uungaji mkono wa kimataifa. Amepangiwa kutoa hotuba mbele ya Jukwaa la kimataifa la majadiliano ya usalama la Shangri-La kesho jumapili.